Arthritis ni neno pana la kiingereza lenye kufunika kundi lenye magonjwa zaidi ya 100. Neno “arthritis” humaanisha “uvimbe kwenye maungio.”Uvimbe ni hali ya asili ya mwili wako kustuka na ugonjwa au jeraha. hujumuisha kuumuka, maumivu, na ugumu. Uvimbe unaodumu kwa kipindi kirefu au unaorudi, kwenye arthritis, unaweza kupelekea uharibifu wa tishu.
Ugonjwa huu wa arthritis umepata kumuona au kusikia ukiitwa kwa jina la kiswahili kama Baridi Yabisi.
Maungio ni pale mifupa miwili au zaidi imekutana, kama vile nyonga au goti.
Mifupa kwenye maungio yako imefunikwa na kitu laini, kama sponji kiitwacho cartilage (inasomeka: katileji ). Husaidia mifupa kwenye maungio kwenda bila kusababisha maumivu.
Kwenye maungio ( joint) kuna kuta iitwayo synovium. Kuta ya synovium huzalisha kimiminika chenye utelezi — kinaitwa synovial fluid — ambacho husaidia maungio kuzuia misuguano kwa ndani.
Kwa nje kuna kifuniko kigumu kinaitwa joint capsule. Kamba kamba zenye nguvu za tishu ziitwazo ligaments, huunganisha mifupa na kusaidia kuweka maungio imara. Misuli na tendons pia hushikilia maungio na kukuruhusu kufanya mwendo.
Ikiwa ni arthritis, eneo la ndani au kuzunguka maungio huumuka, husababisha maumivu, ugumu, na wakati mwengine, mwendo wa shida. Kuna aina ya arthritis pia huathiri maeneo mengine ya mwili, kama vile ngozi na viungo vya ndani ya mwili.
Kiasi cha mtu mmoja kwenye watu wazima watano ana aina mojawapo ya ugonjwa wa arthritis. Ugonjwa huu unaweza kutokea kwa mtu yeyote, lakini huwa ni kawaida unapozeeka.
Aina za Arthritis
Baadhi ya aina za ugonjwa wa arthritis zinazofahamika ni:
Osteoarthritis. Hii ni aina inayofahamika zaidi. Husababisha cartilage mwishoni mwa mifupa yako kulika. Ambapo hupelekea mifupa kusuguana yenyewe. Unaweza kupata maumivu kwenye vidole vyako, magoti au nyonga.
Kuvunjika kwa cartilage, au kufa kabisa,kwa osteoarthritis mara nyingi hutokea ukizeeka. Hii ndio maana osteoarthritis muda mwengine huitwa ugonjwa wa maungio wa wazee. Lakini kuna visababishi vingine, inaweza kuanza mapema sana.kwa mfano jeraha linalotokana na mwana michezo au ufa Karibu na maungio kunaweza kupelekea Inaweza kutokea kwenye maungio yoyote lakini mara nyingi hutokea huathiri viganja maungio yanayo beba uzito kama vile goti, nyonga na maungio ya pingili za uti wa mgongo
Rheumatoid arthritis. Ugonjwa huu unaodumu muda mrefu unaweza kuathiri maungio sehemu yoyote ya mwili lakini mara nyingi huusisha viganja, viwiko na magoti. Kwenye rheumatoid arthritis, mfumo wa Kinga mwilini — ambao huulinda mwili dhidi ya magonjwa– hushambulia maungio kimakosa na kusababisha uvimbe/kuumuka. Uvimbe husambaa hadi kwenye tishu za karibu na unaweza kuharibu cartilage na mfupa. Kwenye hali mbaya zaidi, rheumatoid arthritis inaweza kuathiri maeneo mengine ya mwili, kama vile ngozi, macho, na neva za fahamu.
Gout. Hii ni hali yenye maumivu ambayo hutokea kipindi mwili umeshindwa kuondoa kitu asilia kiitwacho uric acid. Uric acid iliyozidi hutengeneza mawe yenye mfanano wa sindano kwenye maungio ambapo husababisha uvimbe wenye kujaa na maumivu makali. Mara nyingi Gout huathiri kidole gumba cha mguuni, goti, na maungio ya kiganja cha mkono ( wrist joints ).
Nini Kinasababisha Arthritis?
Sababu ya aina nyingi ya magonjwa haya ya arthritis haijulikani. Watafiti wanatazama kwenye kesi ya kurithi na mfumo wa maisha kwenye maendeleo ya arthritis.
Kuna vitu kadhaa ambavyo vinaweza kukuhatarishia kupata ugonjwa wa arthritis, vikiwemo:
Umri. Baada ya muda, maungio yako hulika. Ndio sababu kwanini kuna uwezekano wa kupata arthritis unapozeeka, hasa osteoarthritis.
Jinsi. Karibia aina zote za arthritis huwatokea wanawake, isipokuwa kwa gout.
Genetics. Baadhi ya aina ya arthritis hushambulia familia. Matatizo kama rheumatoid arthritis, lupus, na ankylosing spondylitis, kwa mfano, huambana na aina fulani ya vinasaba.
Uzito uliokithiri. Ukiwa na uzito uliokithiri unashinikiza mkandamizo kwenye maungio yanayobeba uzito wako, unapelekea maungio kusagika na kulika na hatari ya kupata ugonjwa wa arthritis, hasa osteoarthritis.
Majeraha. Yanaweza kusababisha uharibifu wa maungio ambao unaweza kuleta aina mojawapo ya ugonjwa.
Maambukizi. Bacteria, virusi, au fungus wanaweza kuambukiza maungio na kuamsha uvimbe.
Kazi. Kuna aina ya kazi ambazo hutumia miendo ya kujirudia au kunyanyua vitu vizito kunaweza kukandamiza maungio au kusababisha jeraha, ambalo linaweza kupelekea kupata ugonjwa wa arthritis, hasa osteoarthritis. Kwa mfano, kama unahitajika kukunja goti mara nyingi au kuchuchuma ukiwa kazini, kuna uwezekano wa kupata osteoarthritis.
Dalili
Aina tofauti tofauti za arthritis Zina dalili tofauti ambazo zinatofautiana kwenye ubaya kutoka kwa mtu mmoja hadi mwengine. Kwa kawaida Osteoarthritis haisababishi dalili yoyote nje ya maungio. Dalili za aina nyinginezo za arthritis zinaweza kuwa uchovu, homa, kipere,na alama za uvimbe wa maungio, ziliwemo:
- Maumivu
- Kuvimba
- Ukavu/ugumu
- Kuhisi maumivu kila utakapo gusa eneo hilo (tenderness)
- Kubadilika rangi nyekundu kwenye maungio
- Kwenye maungio kunakuwa na joto
- Maungio kuharibika
Ugonjwa wa Arthritis unapimwa vipi?
Upimaji wa ugonjwa wa arthritis ni hatua ya kwanza kuelekea kwenye vipimo. Daktari wako ata:
Zingatia historia yako ya matibabu. Hii itajumuisha maelezo ya dalili zako.
Fanya jaribio la kimwili. Daktari wako atatazama maungio yalivyoumuka, atabonyeza kama panauma, wekundu, joto, au kupotea kwa mwendo kwenye maungio.
Tumia majaribio ya picha kama X-ray. Zoezi hili mara nyingi hueleza ni aina gani ya arthritis unayo. X-ray hutumika kuitambua arthritis, mara nyingi inaonyesha kupotea kwa cartilage, ute wa mifupa, na kwenye kesi mbaya, mifupa kusuguana yenyewe.
Pima kimiminika cha kwenye maungio. Muda mwengine daktari atachukua kimiminika kilichopo kwenye maungio kwa kutumia sindano na kutoa kiasi kidogo cha kimiminika ( joint aspiration ) pamoja na kipimo cha damu hutumika kujulisha osteoarthritis kutoka kwenye aina nyinginezo za arthritis.
Kama daktari wako akituhumu maambukizi ya arthritis tatizo tata la ugonjwa mwengine, kipimo cha kimiminika kutoka katika maungio yaliyo athirika mara nyingi yatathibitisha kipimo na kuamua itatibiwa vipi.
Pima damu au mkojo wako. Vipimo hivi vinaweza kusaidia kumjulisha daktari wako aina gani ya arthritis unayo au ni ugonjwa mwengine ndio sababu ya dalili zako.
Vipimo vya damu kwa rheumatoid arthritis hujumuisha kimoja kwa vimelea vya magonjwa viitwavyo rheumatoid factors (RF), ambavyo watu wengi wenye rheumatoid arthritis wanavyo kwenye damu yao, ijapokuwa RF vinaweza kupatikana kwenye magonjwa mengine.
Kipimo kipya kwa rheumatoid arthritis ambacho kinapima viwango vya vimelea vya ugonjwa kwenye damu (kinaitwa kipimo cha anti-CCP) kina uhakika zaidi na kinafanya kazi kwa ufanisi wa juu zaidi kwa watu wenye au wanaokaribia kupata ugonjwa wa arthritis. Uwepo wa vimelea vya anti-CCP pia hutumika kubashiri watu gani watapa rheumatoid arthritis kwa kiasi kikubwa.
Ugonjwa wa Arthritis Unatibiwa Vipi?
Lengo la matibabu ni kuondoa maumivu, kuongeza au kurahisisha mwendo wa maungio na uwezo, na kuudhibiti ugonjwa kwa namna inavyowezekana. Daktari wako ana machaguzi mengi kukusaidia kudhibiti maumivu, kuzuia uharibifu wa maungio, kuondoa uvimbe.
Matibabu ya arthritis yanaweza kuusisha mapumziko, physical therapy, madawa, uvaaji wa vifaa vya kuzuia maungio, mazoezi, na muda mwengine upasuaji, ili kuweka sawa maungio yaliyo haribika.
Tiba Mbadala
Watu wengi wamegeukia kwenye tiba asilia baada ya kutopata afueni hospitali. Kumekuwa na kubwa ya watu waliopata afueni kutokana na tiba mbadala kwenye dawa za asili.
Kutoka Pandex Herbs, watafiti, watengenezaji na wauzazi wa dawa za asili wameluja na hii dawa tunayoipendekeza: Goutex Powder
Tuma Ujumbe