futa ya Mnyonyo yanaweza kufanya kazi kama kiamshi kilainishi kuondoa tatizo la kutopata choo. Hata hivyo, baadhi ya watu, kama wale ambao wanatumia dozi ya dawa fulani au ambao wana matatizo fulani ya kiafya, wanahitaji kuyaepuka.
Kipindi una shida ya kupata choo, ratiba yako ya kupata choo haiendi kama inavyotakiwa, au kinyesi chako ni kigumu kutoka.
Ni muhimu kuweka akilini kwamba kila mmoja huenda chooni kwa ratiba tofauti. Baadhi ya watu wanaweza kupata choo mara kadhaa kwa siku, ambapo wengine wanapata choo mara 1 kwa siku au huenda chooni kila baada ya siku 2.
Kupungua kokote kwa mwenendo wa kupata choo ambao sio kawaida kwako inawezekana ikawa alama ya tatizo la kutopata choo. Tatizo linaweza kupelekea kupata maumivu ya tumbo na kuvimbiwa
Kutopata choo kunaweza pia kusababisha na kinyesi kigumu, ambacho kinaweza kukulazimsha kujikamua kipindi ukienda chooni.
Mafuta ya Mnyonyo yanaweza kusaidia kama dawa ya muda mfupi kwa tatizo la kutopata choo.
Mafuta ya mnyonyo yametoka kwenye mbegu za mmea wa mnyonyo. Watu wamekuwa wakitumia mafuta haya kama kilainishi kwa maelfu ya miaka, lakini wanasayansi wameanza kufanyia utafiti hivi karibuni kazi zake hasa kwenye mwili.
Watafiti wamegundua kwamba ricinoleic acid, fatty acid iliyosheheni kwenye mafuta ya mnyonyo, hujishikiza kwenye seli za misuli laini ya kuta za utumbo.
Pale ricinoleic itakapofyonzwa kwenye kuta hizi, husababisha misuli hiyo kusinyaa na kusukuma kinyesi, kama vilainishi (laxatives) vifanyavyo. Hii inamaanisha inaweza pia kuwa chanzo cha faida cha kuaminika kwenye kuondoa tatizo la kutopata choo (constipation).
Mafuta ya mnyonyo yana athari sawa kwenye mji wa mimba (uterus), hii ndio maana yamekuwa yakitumika kupunguza uchungu wa uzazi.
Mafuta ya mnyonyo ni kimiminika ambacho unakunywa. Watu wazima na watoto walio juu ya umri wa miaka 12 wanaweza kunywa kati ya vijiko 1 – 4 vya mezani (mililita 15 -60 (mL)) kwa siku kutibu tatizo linalo jirudia la kutopata choo.
Mafuta yanaweza kuwa na ladha chungu. Kupunguza hili, jaribu kuyaweka kwenye jokofu (fridge) kwa muda wa angalau saa 1 yapoe. Halafu yachanganye kwenye glass yenye iliyojaa juice ya matunda. Unaweza pia kununua Mafuta ya mnyonyo yaliyowekwa ladha nzuri yalipotengenezwa.
Mafuta ya Mnyonyo hufanya kazi kwa haraka sana. Unatakiwa uone matokeo ndani ya masaa 6 hadi 12 baada ya kuyanywa. Kwakuwa yanafanya kazi kwa haraka, si wazo zuri kunywa muda mfupi kabla ya kulala.
Kama ilivyo kwa dawa nyingine za kulainisha choo, mafuta ya mnyonyo hayatakiwi kutumia kwa kipindi cha muda mrefu. Baada ya muda mrefu kidogo, yanaweza kupunguza ufanisi wa kazi ya misuli kwenye utumbo wako na kupelekea tatizo sugu la kutopata choo. Kama ukiendelea kupata tatizo la choo kigumu, zungumza na daktari wako.
Kuna watu wanaweza kupata athari hasi kutokana na mafuta ya mnyonyo, ndio maana hayashauriwi kutumiwa na kila mtu. Wakiwemo:
- Wanawake wajawazito, kwani mafuta ya mnyonyo yanaweza kusababisha mji wa mimba (uterus) kusinyaa.
- Matumizi ya mara kwa mara kwa watoto chini ya umri wa miaka 12
- Wale wenye matatizo fulani ya kiafya, kama uvimbe kwenye utumbo (inflammatory bowel disease (IBD)) na kidole tumbo (appendicitis)
- Watu wazima zaidi ya miaka 60, kwani mafuta ya mnyonyo yanaweza kuhatarisha tatizo la mwendo wa chakula kwenye njia yake .
Unahitaji kujizuia kunywa mafuta ya mnyonyo kama upo kwenye dozi ya dawa fulani, ikiwemo:
- diuretics, ambazo zinaweza pia kushusha kiasi cha madini ya potassium kwenye mwili wako
- antibiotics, ikiwemo tetracycline
- blood thinners
Kwa nyongeza ya ladha yake mbaya, mafuta ya mnyonyo yana madhara. Kama vilanisha choo vyengine, yanaweza kusababisha maumivu ya tumbo na kuharisha. Yanaweza pia kushusha ufyonzwaji wa virutubisho kwenye utumbo. Ijapokuwa, hii hutokea kipindi yanapotumika kwa wingi.
Sababu za choo kigumu mara nyingi huusiana na chakula. Kama hupati fiber na maji ya kutosha, kinyesi chako huwa kigumu na kikavu. Inapotokea hii, choo chako hakiwezi kutoka kwa urahisi kupitia utumbo wako.
Baadhi ya magonjwa yanaweza kupelekea kuwa na choo kigumu. Baadhi ya magonjwa hayo ni:
- multiple sclerosis
- Ugonjwa wa Parkinson’s
- stroke
- Ugonjwa wa kisukari ( diabetes )
- Ugonjwa wa Rovu (hypothyroidism)
- Ugonjwa uliokithiri wa figo
- Kansa ya utumbo
Baadhi ya madawa ya tiba yanaweza kusababisha choo kigumu kama athari zake hasi. Madawa hayo ni kama yafuatayo:
- Dawa za kushusha acid tumboni (antacids)
- Dawa za kupunguza ukali wa kifafa
- Dawa zinazoshusha presha ya damu
- Virutubisho vya madini joto (iron supplements)
- Madawa ya kulevya ya kuondoa maumivu
- sedatives
- Baadhi ya antidepressants
Kuna watu hupata choo kigumu mara kadhaa. Wenye ujauzito wanaweza kupata choo kigumu kama matokeo ya mabadiliko ya kihomoni. Mwendo wa chakula kwenye njia yake hupungua kadri umri unavyoongezeka, na kuwaacha baadhi ya wazee watu wazima wakipata tatizo sugu la choo kigumu.
Kuzuia Choo Kigumu
Mara nyingi, njia nzuri ya kuzuia choo kigumu ni chakula bora na mazoezi. Amua kufanya yafuatayo kwenye maisha yako ya kila siku:
Kula fiber kwa wingi: Fiber( nyuzi nyuzi ) hulainisha choo na husaidia kupita kwa urahisi kwenye utumbo. Lenga kula gram 14 (gm) za fiber kwa kila kalori 1000 unazokula, na kunywa vimiminika kwa wingi kulainisha choo chako.
Changamka: Inaweza pia kusaidia ukiwa mchangamfu katika siku nyingi za wiki . Kama ilivyo kwa mazoezi yanavyofanya kazi kwenye misuli na miguu yako, pia huimarisha misuli kwenye utumbo wako.
Kwenda chooni kwa mpangilio: Inapowezekana, jaribu kwenda chooni kwenye muda mmoja kila siku. Ni muhimu kutoharakisha na jipe muda chakula kishuke vizuri.
Maswali Yanayoulizwa Mara kwa MaraKiasi gani cha mafuta ya mnyonyo mtu mzima anaweza kunywa kutibu choo kigumu?
Watu wazima wanaweza kunywa dozi ya kijiko kimoja hadi vinne ( mL 5 hadi mL 15 ) kwa mara moja kwa siku vya mafuta ya mnyonyo kutibu choo kigumu.
Kiasi gani cha mafuta ya mnyonyo watoto wanatakiwa wanywe kutibu tatizo la choo kigumu?
Watoto kati ya umri wa miaka miwili na 12 wanaweza kunywa kwa mara moja kwa siku vijiko vya chai kimoja hadi vitatu ( mL5 hadi mL15 ) vya mafuta ya mnyonyo kwa kutibu tatizo la choo kigumu. Hata hivyo, haitakiwi kutumiwa na watoto chini ya umri wa miaka bila ushauri wa daktari.
Mafuta ya Mnyonyo ni chaguzi lenye athari chanya kwa kupata afueni ya choo kigumu. Husababisha misuli kwenye utumbo wako kusinyaa na kusukuma choo nje.
Hata hivyo, huja na madhara yake na si nzuri kwa kila mtu. Mafuta ya mnyonyo pia hayashauriwi kwa matibabu ya muda mrefu kutibu choo kigumu.
Kama unapatwa na choo kigumu mara kwa mara na hupati nafuu, Muone daktari kuhusu uchaguzi wa tiba nyingine.
Tutu ( cold Press ) Castor Oil
Tuma Ujumbe