UVIMBE KWENYE KIZAZI NA UGUMBA (FIBROIDS, UTERINE MYOMA
FIBROID NI NINI?
Siku hizi kuna ongezeko kubwa sana la huu ugonjwa hebu tega sikio.
FIBROID ni uvimbe ambao hutokea kwenye kuza za kizazi ambapo uvimbe huu unaweza kuwa ndani ya kizazi(ukutani mwa kizazi) au ndani ya nyama ya kizazi na nje kwenye ukuta wa kizazi.
Uvimbe katika mfuko wa kizazi wa mwanamke hujulikana kama ‘uterine myoma’ au fibroid. Uvimbe huu hutokea kwenye misuli laini ya mfuko wa uzazi.Uvimbe huu hutokea katika sehemu mbalimbali juu au ndani ya mji wa uzazi wa mwanamke.
Ni uvimbe ambao hauhusiani na kansa na unaweza kubadilika rangi ukawa wa njano, unaweza kubadilika ukawa kama maji tu na kurudi tena kuwa mgumu.Uvimbe kwenye kizazi hujulikana pia kwa majina haya kitaalamu: ‘Uterine fibroids’, ‘Myoma’ au ‘fibromyoma’.
Hujulikana pia kama ‘leiomyoma’ katika lugha ya kidaktari. Wanawake wenye umri kati ya miaka 30 hadi 50 ndiyo wanapatwa kirahisi zaidi na ugonjwa huu.
SABABU ZA MWANAMKE KUPATA UVIMBE KWENYE KIZAZI.
Chanzo cha moja kwa moja cha ugonjwa huu bado hakijulikani wazi, hata hivyo baadhi ya sababu za kutokea huu uvimbe ni pamoja na;
1. Kuongezeka sana vichocheo vya progesterone na estrogen kuzidi kiwango mwilini.
2. Ujauzito kwasababu ya kupanda kwa vichocheo vya Estogen
3. Uzito/ unene kupita kiasi.
4. Jenetiki zisizo za kawaida (Genetic Disorders)
5. Mfumo usio sawa wa mishipa ya damu.
6. Sababu za kurithi.
7. Lishe isiyo sawa/Lishe duni.
8. Sumu na taka mbalimbali mwilini.
9. Mvurugiko wa vichochezi (Hormonal imbalance)
AINA ZA UVIMBE KWENYE KIZAZI
Kuna aina kuu 3 za uvimbe kwenye kizazi kama ifuatavyo:
1. Submucosal fibroids (ndani ya tabaka la kizazi)
2. Intramural fibroid (ndani ya nyama(misuli) ya kizazi)
3. Subserosal(nje ya kizazi)
WAFUATAO WAPO HATARINI KUPATA UVIMBE KWENYE KIZAZI(UTERINE FIBROID)
1. Mwanamke ambae hajawahi kupata mtoto mpaka umri mkubwa
2. Miaka kuanzia kubalehe mpaka hedhi kukoma
3. kurithi
4. Unene/uzito kupita kiasi
5. kuingia hedhi mapema
Fibroids sio kansa ni uvimbe wa kawaida tu ambao unakua kwa kutegemea kichocheo cha estrogen hormone ndio maana kuanzia kubalehe mpaka kukoma kwa hedhi ndio wako hatarini.Na mara nyingi uvimbe huu huwa unaongezeka kukua sana hasa wakati wa ujauzito kwani vichocheo hivi huongezeka wakati huu kulinda makazi ya mtoto.Ni watu waliofikia kikomo cha hedhi hawapati fibroids au kitaalam leomyoma kwasababu vichocheo vya Estogen hushuka chini.
DALILI ZA MWANAMKE MWENYE UVIMBE KWENYE KIZAZI (UTERINE FIBROIDS):
1. Kupata damu nyingi wakati wa hedhi.
2. Maumivu makali wakati wa siku za hedhi.
3. Kuvimba miguu (lower limb oedema)
4. Unaweza kuhisi una ujauzito.
5. Maumivu wakati wa tendo la ndoa.
6. Kuhisi kuvimbiwa.
7. Kupata haja ndogo kwa taabu (Difficulty in passing urine)
8. Kutokwa na uchafu ukeni.
9. Kupata choo kigumu au kufunga choo (Constipation)
10. Maumivu nyuma ya mgongo.
11. Maumivu katika miguu ikiwa ni pamoja na miguu kuwaka moto.
12. Upungufu wa damu.
13. Maumivu ya kichwa.
14. Uzazi wa shida.
15. Kutopata ujauzito.
16. Kuvimba sehemu ya chini ya tumbo.
17. Maumivu ya nyonga.
18. Mimba kutoka/kuharibika mara kwa mara (miscarriage).
19. Kukojoa mara kwa mara kwani uvimbe huweka mgandamizo katika kibofu cha mkojo
20. Hedhi zisizokuwa na mpangilio
21. Tumbo kujaa gesi
MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUPONA HARAKA UVIMBE KWENYE KIZAZI (Uterine fibroid).
1. Hakikisha una uzito sawa kila mara kulingana na urefu wako.
2. Kula sana mboga za kijani na matunda
3. Fanya mazoezi ya viungo kila mara, mara 4 mapaka 5 kwa wiki
4. Kunywa maji mengi kila siku lita mbili mpaka lita tatu
5. Kula sana vyakula vyenye nyuzi nyuzi (faiba) na punguza vyakula vilivyokaangwa,vyakula vya wanga na Sukari
6. Usitumie bidhaa zozote zenye Caffeine (chai ya rangi, kahawa, soda nyeusi zote nk), punguza matumizi ya nyama nyekundu na vyakula vya kuchomwa au kupikwa katikati ya mafuta mengi (maandazi, chipsi, nk)
7. Achana kabisa na mawazo mawazo (stress) na hamaki nyingine zozote
8. Acha kuvuta sigara/tumbaku na vilevi vingine vyote hadi hapo utakapopona kabisa
0656 198 441
DAR ES SALAAM, ILALA.
Tuma Ujumbe