PELVIC INFLAMMATORY DISEASE (PID) NA UGUMBA (Infertility)
-Ni maambukizi katika viungo vya uzazi vya mwanamke.Na maambukizi haya kutokea ikiwa bacteria wanaoambukiza kwa njia ya kujamiiana watasambaa kutoka kwenye Uke kwenda kwenye mji wa mimba (Uterus),Mirija ya uzazi na kwenye Ovary (ambapo mayai ya mwanamke hupatikana).
-Maambukizi ya PID mara nyingi husababishwa na Bacteria wanaosababisha Ugonjwa wa Kisonono na Chlamydia.Hivyo wanawake wenye Kisonono wapo hatarini zaid Kupata PID
DALILI ZA MWANAMKE MWENYE PID (PELVIC INFLAMMATORY DISEASE)
-Zifuatazo ni dalili za mwanamke Mwenye PID:
⏬⏬⏬⏬
1. Maumivu ya kawaida ama makali chini ya kitovu.
2. Kutokwa Uchafu usio wa kawaida Ukeni ambao ni mzito wenye HARUFU MBAYA wenye rangi ya maziwa ama njano.
3. Maumivu makali wakati wa kujamiiana.
4. Hupata homa(joto laweza kupanda mpaka 110 F (38.3 °C).
5. Maumivu makali wakati wa kukojoa na hupelekea Kupata ugumu wakati wa kukojoa.
6. Hupatwa na kichefuchefu.
7. Kutapika
8. Miwasho sehemu za
siri
9. Uchovu
10. Uke kuwa mlaini sana
11. Kizunguzungu
12. Kutokwa na maji maji ukeni kupita kiasi.
13. Kuvurugika kwa Hedhi
ATHARI/MDHARA YA PID
1. Ugumba kwa wanawake
2. Kupata Kansa ya shingo ya Uzazi.
3. Kutunga mimba nje ya kizazi kutokana na yai kushindwa kufika katika mji wa mimba kutokana na madhara ya PID katika mirija ya Uzazi.
4. KUSABABISHA majeraha nje na ndani ya mirija ya uzazi na hii hupelekea kuziba kwa mirija ya Uzazi.
5. Maumivu ya tumbo /ngonga mara kwa mara baada ya tendo la ndoa na kipindi cha uchavushwaji mayai (Ovulation).
6. Kuziba kwa mirija ya uzazi (Fallopian tubes blockage)
7. Mirija ya uzazi kujaa maji (HYDROSALPINX)
8. Kuvimba kwa mirija ya uzazi (Salpingitis)
9. Mwanamke hukosa kujiamini kwasababu ya kutokwa na harufu mbaya ukweni na uchafu
10. Migogoro kwenye ndoa na wakati mwingine huweza kusababisha mwanamke kuachwa hivyo kuvunjika kwa ndoa.
JINSI YA KUEPUKA/KUJIKINGA NA PID
1. Epuka kuvaliana nguo za ndani.
2. Kuwa na tabia ya kupima mara kwa mara mfumo wako wa Uzazi.
3. Kuwa msafi wa mwili na nguo zako za ndan
4. Kula lishe bora.
5. Epuka kufanya tendo la ndoa na mwenza wako mara baada ya kugundua ana magonjwa ya kujamiiana (STDs)
6. Fanya vipimo vya magonjwa ya ngono kama Kisonono na Kaswende wewe na mwenza wako kabla ya kuanza Mahusiano.
Dr. Mapande
0656 198 441
Tuma Ujumbe